Friday, December 9, 2011

MWANDISHI BORA MWANANCHI 2011

Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Elias Msuya akikabidhiwa zawadi zake baada ya kutangazwa mshindi katika sherehe za kuaga mwaka zilizofanyika Tabata relini jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kutoka kulia ni Meneja utumishi (HR-Manager) Victoria Muro, Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Sam Shollei, Kaimu mkurugenzi Theophil Makunga na mhariri wa gazeti la Mwananchi Dennis Msaki.



Marafiki zake Elias Msuya wakimshangilia baada ya kutangazwa mshindi

Monday, October 17, 2011

MAMBO YA BUTIAMA

Nimepozi na Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Mwitongo




Kaburi la Mwalimu Nyyerere



Nyumba hii Nyerere aliishi siku 17 tu


Nyumba aliyojengewa mwaka 1974


Gari alilopanda kwa mara ya mwisho

MAMBO YA BUTIAMA

Hili ndilo kanisa alilokuwa akisali Mwalimu Nyerere



Mkurugenzi wa Makumbushio ya Mwalimu Nyerere Emmanuel Kiondo





Hiyo ndiyo suti na viatu alivyokuwa akipenda kuvaa Mwalimu Nyerere

Thursday, September 29, 2011

MGOMO WA MAFUTA MALAWI

Hapa Bongo Ewura wakilala wakiamka wanabadilisha bei za mafuta wanavyotaka
Cheki Wamalawi walivyo active kwenye issue zao. Kudadeki, haipandishwi bei hata senti.









Friday, September 23, 2011

MV SPICE ISLANDER, NANI ALAUMIWE?



Meli ilivyozama



Mbunge wa Ziwani Ahmed Ngwali akiorodhesha majina ya walioathiriwa

Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar Seif Sharif Hamad na maafisa wengine wa serikali hiyo wakiwahami waliofiwa

Elias Msuya
TUKIO la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander lililotokea hivi karibuni katika eneo la Nungwi na kusababisha vifo, majeruhi na watu wengi kupotea, limefufua hisi nyingi za mionmgoni mwa Wazanzibar.
Licha ya serikali ya Zanzibar kutangaza kufanya uchunguzi, maswali mengi yameanza kujitokeza kuhusu utendaji wa serikali hiyo ambayo kwasasa inahusisha vyama vya CUF mna CCM.
Wakazi wa kisiwa cha Pemba ambao kimsingi ndiyo wamepata msiba mkubwa kutokana na ajali hiyo, wameibuka na hisia za kutengwa licha ya chama cha Wananchi (CUF) ambacho ngome yake iko kisiwani humo kuwa serikalini.
Katika msiba huo, wananchi wengi wamepoteza dugu na jamaa zao. Lakini kwa Rashid Abdallah Rashid anayeishi Shehia ya Jadida wilayani Wete msiba huo kwake umekuja mara mbili, kwani ndugu zake waliokuwa wakija kuhani msiba uliotokea kwake, waliishia kufa kwenye ajali hiyo.
Rashid ambaye anasema bado wako kwenye jitihada za kuwatafuta ndugu zao, anasema kuwa kati ya ndugu 30 waliosafiri siku hiyo, hadi sasa wamepata maiti nne na watu walio hai watatu.
“Siku ya Ijumaa tulipata msiba wa dada ambaye alianguka kwenye pikipiki na kugongwa na gari. Kwakuwa kichwa kilisagika vibaya, tulimzika siku hiyo hiyo. Tukawajulisha ndugu zetu wa Unguja na kwingineko waje. Ndiyo hao wameishia kwenye ajali ya Mv Spice Islander” anasema Rashid.
Rashid anaelekeza lawama kwa serikali ya Zanzibar, akisema kuwa imezembea kwakuwa wengi wa abiria waliokuwamo walitoka Pemba.
“Japo ajali hii ilipangwa na Mwenyezi Mungu, kuna uzembe mkubwa uliofanywa na serikali. Tukio hilo lilianzia bandarini, wahusika waliona, taarifa za kuzama kwa meli zilianza kupatikana tangu saa nane kasorobo, serikali haikuchukua hatua yoyote, hadi saa mbili asubuhi zilipoletwa helkopita” anasena Rashid na kuongeza,
“Kama wangekuwa watu wa Bara, Kikwete asingekubali, wangekuwa Waunguja, hatua zingechukuliwa mapema. Lakini kwakuwa sisi ni Wapemba, hatukubaliki siku zote”.
Anaendelea kulalamika kuwa ubovu wa vyombo vya usafiri na usafirishaji vinavyofanya safari zake kisiwani humo, umekuwa ukilalamikiwa kwa muda mrefu, lakini hauchukuliwi hatua yoyote ukilinganishwa na kisiwani Unguja,
“Vyombo tunavyotumia kwa usafiri sisi Wapemba ni vya mizigo. Hakuna hatua zozote zinazochukuliwa, lakini vyombo vinavyofanya safari za Unguja kwenda Dar es Salaam, vinachekiwa kila mara” anasema Rashid.
Naye Mwajuma Omar wa shehia ya Kipangani wilayani Wete ambaye amepoteza watoto wanne na wajukuu wawili katika ajali hiyo, ameilalamikia serikali kwa kutokuwa makini katika ukaguzi wa vyombo vya usafiri,
“Ni kweli serikali itatupa mkono wa pole lakini hatuwezi kuwasahau watoto wetu. Nawashauri tu wawe makini katika kuvikagua vyombo vya usafiri” anasema.
Akisimulia tukio hilo, Mwajuma anasema kuwa watoto wake walikuwa katika meli hiyo na walimpigia simu kuwa wako njiani hadi saa tano usiku, lakini ilipofika saa nane usiku, walimpigia simu baba yao,
“Walipigia siku baba yao kuwa wanakufa, baada hapo hatukuwasikia tena hadi leo. Hatujafanikia hata kupata maiti” anasema.
Baadhi ya wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF) wamechukua hatua ikiwa ni pamoja na kuhakiki wananchi wao walioathiriwa na ajali hiyo. Hata hivyo kilio chao hakina tofauti na wananchi wao.
Mbunge wa jimbo la Ole, Rajab Mbarouk anasema kuwa serikali imeonyesha kuwatenga watu wa Pemba katika msiba huo.
“Tulitarajia viongozi wa serikali kuja huku Pemba kuomboleza na sisi. Lakini tunaona viongozi wote wameishia Unguja, hata hitima wameitolea huko, wakati wenye msiba tuko huku Pemba” anasema Mbarouk.
Mborouk ambaye amefanya tathmini ya wananchi wa jimbo lake waliofariki au kuptea katika ajali hiyo, anasema kuwa atapeleka hoja binafsi Bungeni ili kumwajibisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda,
“Inaonyesha serikali haina takwimu sahihi, ndiyo maana sisi tumeamua kufanya tathimini ya kina. Sisi ni wasemaji wa wananchi siyo serikali. Nina mpango wa kupeleka hoja binafsi Bungeni ili Waziri Mkuu awajibike” alisema Mbarouk na kuongeza,
“Nilishawahi kuuliza swali Bungeni kuhusu usalama wa vyombo vya majini lakini serikali haikuchukua hatua yoyote” anasema.
Mbunge wa jimbo la Ziwani Ahmed Ngwali anasema kuwa anafanya tathmini ya jimbo lake ili afanye utaratibvu wa kuishitaki serikali kutokana na uzembe uliosababisha ajali hiyo,
“Tukishapata orodha kamili ya wananchi, nakwenda kutafuta orodha ya abiria waliokuwa kwenye meli, nalinganisha. Kwa wale waliokuwa na tiketi, nitasimamia walipwe bima zao na mmiliki wa meli. Wale waliozidi nitaishitaki serikali kwa kuzembea” anasema Ngwali na kuongeza,
“Huu ni uzembe na ni lazima twende mahakamani. Ikiwa samaki wa Magufuli (Waziri wa Ujenzi) hadi leo wana wanasotesha watu mahakamani, itakuja kuwa watu?”.
Kwa upande wake Mratibu wa Wazee wa Pemba Ali Makame Issa anasema hadi sasa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, bado haijaonyesha sura yake halisi, kwahiyo siyo rahisi kuona matunda yake mapema,
“Unajua kwa sasa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, bado haijaonyesha sura yale halisi. Utakuta waziri ni wa CUF lakini watendaji wake wote ni wana CCM na bado wana zile chuki za kisiasa” anasema Issa.
Anamtetea Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad, akisema kuwa tukio hilo linaweza kuwa njama kwake,
“Kwasababu yule waziri amechukua hatua mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuzuia meli ya Mv Maendeleo isifanye kazi kwakuwa ilikuwa na kasoro, akazuia Mv Serengeti na Sea Gull hadi zilipofanya marekebisho. Sasa kwa mlolongo huo, inawezekana watendaji wake tu, ndiyo wamefanya hujuma” anasema.
Issa anasema hata nahodha wa meli hiyo ambaye kwa sasa anatafutwa na jeshi la polisi, amepotea katika mazingira ya kutatanisha,
“Inatia shaka kuona kuwa jeshi la polisi linatangaza kumtafuta nahodha baada ya wiki moja, siku zote walikuwa wapi? Huenda wenyewe wanajua aliko” anasema.
Hata hivyo, akizungumzia ajali hiyo, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad anapinga kuwepo kwa njama wala uzembe katika ajali hiyo.
“Nasema ajali ni ajali, imeshatokea na kwa imani ya dini yangu, ni Mungu tu alipanga iwe. Hakuna njama yoyote iliyopangwa” anasema.
Akizungumzia kuwajibika kwake, Waziri Hamad ambaye anatoka chama cha Wananchi, (CUF) anasema yuko tayari kufanya hivyo ila hadi uchunguzi ufanyike kwanza.
“Mimi sihusiki na kukagua meli wala naibu waziri, kuna watendaji kama vile Wakurugenzi, Katibu, Naibu katibu na wengineo. Tusifanye mchezo wa ng’ombe ambapo anayekula ni wa mbele, lakini anapigwa bakora wa nyuma. Tusubiri uchunguzi ufanywe, ndiyo tutajua kama kuna uzembe au hujuma” anasema Hamad.
Hamad amesema kuwa hajakiangusha chama chake cha CUF kwakuwa tukio hilo limetokea kama ajali tu.
Lakini hisia hizo za Wapemba kutengwa na serikali hiyo, zimepingwa na Makamu wa kwanza wa serikali hiyo Seif Sharif Hamad akisema kuwa serikali hiyo imepanga kuwatembelea wote walioathiriwa na ajali hiyo.
“Nimekuja kuwajuli hali kutokana na ajali hii inayotugusa sote. Huu ni utaratibu tuliojiwekea, baada ya kutafakari suala hili, tumeona kwamba mimi nije kwanza, lakini viongozi wote watafika kuwajulia hali” anasema Maalim Seif.
Amekiri kuwepo kwa uzembe uliosababisha ajali hiyo na kusema kuwa serikali itafanya uchunguzi wa kina ili kubaini kasoro zilizokuwepo.
“Kuna kasoro zilizochangia ajali hiyo, kuna kasoro kwa wenye chombo, kuna kasoro kwa serikali hasa watu wenye dhamana hiyo, lakini hatutaki tuhukumu bila ushahidi. Tutafanya uchunguzi na matokeo yake yatawekwa hadharani kila mtu aone. Kama serikali au kama ni mtu yoyote awajibike.
Kuhusu jitihada za serikali ya Zanzibar, Maalim Seif anasema kuwa serikali hiyo kwa sasa ina mpango wa kuleta meli nyingine mpya ili kupunguza adha ya usafiri wa majini.
“Kwa sasa serikali ina mpango wa kununua meli mpya. Siyo hizi ‘boat’, tunataka meli zilizozoeleka na Wazanzibar. Mtu akitaka kuingia na mizigo yake na watu wake waingie kwa wingi” anasema Maalim Seif.

Tuesday, September 6, 2011

FRIENDS ON FRIDAY YAFANA

Baadhi ya picha zikionyesha Mchungaji Steven Wambura aki perfrom huku mashabiki wakimfuatilia katika tamasha lililofanyika Tamal Hotel Mwenge Dar, majuzi.



Thursday, August 4, 2011

AgriSol ni wawekezaji au wamekwenda kupora ardhi Mpanda?



AgriSol ni wawekezaji, au wamekuja kupora ardhi ya Mpanda?

Elias Msuya

KAMPUNI ya kimarekani ijulikanayo kama AgriSol Energy LLC inakamilisha taratibu za kumilikishwa na serikali ardhi ya hifadhi iliyopo katika wilaya ya Mpanda, mkoani Rukwa, uchunguzi umebaini.
Taarifa za awali zinaonyesha kuwa, ardhi inayotarajiwa kumilikishwa kwa kampuni hiyo inahusisha zilipo kambi za wakimbizi za Katumba yenye ekari 80,317 na Mishamo yenye ekari 219,800 na kambi ya Lugufu iliyoko mkoani Kigoma yenye ekari 25,000.
Mmoja kati ya washirika wa karibu wa kampuni hiyo nchini ni aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Idd Simba ambaye ndiyo kiongozi wa Agrisol ya Tanzania yenye ofosi zake Mikocheni A Dar es Salaam. Mshirika mwingine nchini ni kampuni ya Serenge Advisers Limited” alisema Baha.
Katika waraka wake ambao Mwananchi imefanikiwa kuuona, Idd Simba anaitetea kampuni hiyo ya Marekani akisema kuwa taarifa zake zimekuwa zikipotoshwa na watu wengine,
“Habari za hivi karibuni zimekuwa zikipotosha nia yetu. Nikiwa kama mhusika wa Agrisol Tanzania tangu mwanzo najua watu, mipango, siasa na faida za mradi huu kwa Tanzania. Mradi wetu umelenga kuwashirikisha wakulima wa ngazi ya juu wa dunia na kuifanya ardhi ya Tanzania kuwa katika viwango vya juu na matumizi stahiki” anasema Idd Simba katika waraka huo.
Washirika wengine wa Agrisol ni pamoja na taasisi ya Pharos Global Agricultural Fund iliyo chini ya Pharos Financial Group ya Dubai inayoongozwa na Peter Halloran.
Nyingine ni Summit Group yenye makao makuu Iowa Marekani ikijishughulisha na kilimo na ufugaji na Chuo kikuu cha Iowa kinachoheshimika kwa masuala ya ardhi nchini humo. Chuo hicho kimepewa kazi ya kufanya upembuzi yakinifu ukiwamo wa udongo, hali ya hewa, mvua na hali ya eneo zima.
Tayari serikali imeshafanya makubaliano ya awali (Memorandum of understand) na kampuni hiyo.
Katika makubaliano hayo (tunao) Kuna mambo kadhaa yenye utata katika makubaliano hayo. Kwamfano malipo ya umilikishwaji wa ardhi hiyo ni madogo mno ambapo AgriSol Energy watatakiwa kulipa ada ya sh 200 na ushuru kwa halmashauri sh 500 kwa eka moja.
Vile vile wanamilikishwa eneo hilo kwa muda wa miaka 99 muda unaolalamikiwa na watu wengi kuwa ni mrefu mno.
Vilevile, kampuni hiyo kutumia wafanyakazi kutoka nje ya nchi hivyo kuwakosesha ajira wazawa.
Kampuni hiyo inayojihusisha na kilimo na ufugaji, kwa sasa inaishawishi serikali ibadilishe sera zake ili iruhusiwe kulima mazao yaliyorekebishwa viini tete (GMO).
Halafu kama kutatokea mgogoro, usuluhishi wake utakwenda kufanywa nchini Uingereza kwa sheria zao.
Nimezumza na Mkurugenzi wa wilaya hiyo Mhandisi Emmanuel Kalobero ambaye anakiri kuwepo kwa makubaliano hayo na kubainisha kuwa kampuni hiyo ilifika wilayani hapo na kuliona eneo lenyewe. Kisha ikawachukua baadhi ya maafisa wa wilaya hiyo na kuwapeleka Iowa Marekani ili kujionea yalipo makao makuu ya yake.
Anawataja maafisa hao kuwa ni pamoja na mkuu wa wilaya ya Mpanda Dk Rajab Rutenge, katibu tawala wa mkoa wa Rukwa Salum Chima, mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda Philip Kalyalya, Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Sylvestre Swima, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Emmanuel Kalobero, Diwani na mjumbe wa kamati ya fedha Rose Malyalya, Diwani na mwenyekiti wa kamati ya maadili Teddy Nyambo, mwanasheria wa Halmashauri Patrick Mwakyusa, Afisa kilimo Fabian Kashindye na Haruna Mwalutanile.
Naye mwanasheria wa halmashauri ya Mpanda Patrick Mwakyusa, halmashauri hiyo ilipata agizo kutoka serikalini ya kuandaa maeneo husika kwaajili ya uwekezaji,
“Mnamo Februari mwaka 2010 tuliandikiwa kutoka mkoani tukiambiwa kuwa kuna mwekezaji (Agrisol) atakuja kuchukua maeneo ya makambi ya wakimbizi” anasema Mwakyusa na kuongeza,
“Maeneo hayo yalianza kukaliwa na wakimbizi tangu mwaka 1972 katika eneo la Katumba, mwaka 1978 wakimbizi wa Burundi waliokuwa Ulyanhulu walipozidi ndiyo wakahamishiwa eneo la Mishamo. Sisi kama Halmashauri hatuma maamuzi na maeneo hayo, tunapokea maelekezo tu”.
Mwakyusa anasema kuwa mwaka 2008, kampuni ya Agrisol ilikuja kufanya mazungumzo na serikali na mwaka 2010 kampuni hyo ilikuja wilayani humo kuangalia ubora wa udongo.
“Mazungumzo yalilenga kufanya utafitio na kuweka makubaliano kwamba uwekezaji utaanza baada ya serikali kuwaondoa wakimbizi, kufuatwa kwa sheria za ardhi na kwamba vijiji vya Watanzania vinavyozunguka kambi hizo vilindwe” anasema.
Anavitaja baadhi ya vijiji hivyo kati ya vingine 27 kuwa ni pamoja na Ndui Station, Laini, Kambuzi na Litapunga. Alisisitiza kuwa hata maeneo yenye shule za msingi na sekondari na zahanati hayataguswa.
Alisema kuwa mkataba rasmi utaingiwa Agosti mwaka huu na kwamba Halmashauri itafaidika kwa kutumia sheria za ushuru za ndani.
“Watakuwa wakilipa ushuru mara mbili kwa kila ekari ambapo ekari moja itakuwa ni sh 200 na ushuru wa sh500 kwa Halmashauri . Jamii zinazozunguka zitapata ajira, ujuzi na masoko ya bidhaa zao” anasema.
Kuhusu suala la muda wa mkataba, Mwakyusa anakiri kuwa hiyo ni changamoto watakayoizungumza wakati wa kusaini mkataba.
Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya hiyo, Lauteri Kanoni anakiri kuhusishwa kwenye mkataba huo na kusemakuwa kampuni hiyo inajitosheleza kufanya uwekezaji mkubwa katika kilimo.
Anapinga suala la wafugaji kutoka mikoa mingine kuingiza mifugo wilayani humo akisema kuwa hawana utaratibu mzuri,
“Hatutaki kupokea mifugo kutoka nje ya mkoa huu. Tumeshafanya sensa na mifugo iliyopo inatosha. Eneo hilo tutawapa Agrisol kwasababu wana uwezo wa kuliendeleza, siyofugaji wasio na utaratibu mzuri” anasema.
Naye mkuu wa wilaya hiyo Dk Rajab Rutenge anasema kuwa hana wasiwasi na wawekezaji hao kwakuwa wataleta faida kubwa,
“Hatuna wasiwasi nao kwasababu wataleta faida kubwa. Mimi mtaalamu wa usalama wa chakula, Tanzania bado tuna uhaba wa chakula, tukiwaakila watu kama hao watazalisha chakula cha kutosha kumaliza tatizo la njaa” anasema.
Akizungumzia suala la mbegu zilizoboreshwa (GMO), Dk Rutenge anasema kuwa hilo pia siyo tatizo kwani tayari mazao hayo yalishaingizwa nchini tangu zamani,
“GMO siyo tatizo, mbona miaka ya 1980 tulikula unga wa yanga na Bulgur? Hizo si zilikuwa GMO? Nadhani suala la msingi ni kuwaelimisha wakulima. Vilevile wawekezaji hao wafuate sheria zetu” anasema Dk Rutenge.
Kwa mujibu wa tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Septemba 2010, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitembelea Marekani ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea kampuni ya AgriSol Energy LLC yenye makao yake katika jimbo la Iowa
Lakini hivi karibuni suala hilo limeibuka Bungeni mjini Dodoma ambapo kambi rasmi ya upinzani Bungeni imehoji uwekezaji huo.
Akijibu hoja hizo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda anakiri mpango wa kuwamilikisha AgriSol eneo hilo akisema kuwa ni hatua ya kuimarisha uchumi wa mikoa ya Rukwa na Kigoma.
“Mimi natoka Mpanda na wananchi waliopo katika maeneo hayo ni wananchi wangu. Nikimsikia mtu anazungumzia suala hilo nashangaa, wale ni wapiga kura wangu” anasema na kuendelea,
“Kwa muda mrefu mikoa ya Rukwa na Kigoma imekuwa nyuma kwa kila kitu, si barabara ambapo lami inawekwa kwenye madaraja tu, hata kiuchumi. Tunalisha nchi nzima lakini hatuna kitu. Tulichofanya ni kuwarudisha wakimbizi kwao Burundi kwakuwa nchi yao sasa ina demokrasia. Sasa tunafanya nini kama kuna watu wanataka kuwekeza?”.
Waziri Mkuu Pinda anakanusha madai kuwa tayari kuna mkataba kati ya AgriSol na Halimashauri ya Mpanda, badala yake anasema kilichofikia ni makubaliano tu ya awali.
Ameongeza kuwa baada ya kufanya utafiti wa udongo, watalifikisha suala hilo kwenye kituo cha uwekezaji (TIC) na Wizara ya ardhi.
Wananchi wa Mpanda wanapinga
Licha ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuonyesha mzigo wa kuwatetea wananchi wake katika uwekezaji huo huku Halimashauri ya wilaya ya Mpanfa ikiutetea, wananchi wengi katika wilaya hiyo hawaelewi kinachoendelea na wengine wanaoelewa wanaipinga AgriSol.
Nimezungumza na mkuu wa kambi za wakimbizi za Katumba na Mishamo Athuman Igwe ambaye ameonyesha kuutilia shaka uwekezaji huo kwasababu mbili,
“Kwanza muda wa miaka 99 wanaopewa kumiliki ardhi yenyewe ni mrefu mno. Ni mkataba wa kikoloni, mambo yakiharibika itakuwa vigumu kujinasua.
Pili, ardhi yenyewe imechoka sana. Labda watumie mbolea nyingi kuiorutubisha. Au pengine kuna kitu wanakitafuta zaidi ya kilimo” anasema Igwe.
Naye diwani wa kata ya Litapunga yenye vijiji vya Kambuzi Holt, Litapunga na Ndui, Godfrey Lusambwa anasema kuwa ataupinga mkataba huo kwakuwa hakushirikishwa kama diwani,
“Huo uwekezaji nimeusikia kwenye vikao vya madiwani na tumeambiwa tuwahasishe wananchi. lakini kwenye vikao halisi vya makubaliano sikuhusishwa.kwamfano mkutano wa uwekezaji uliohudhuriwa na Waziri Mkuu Pinda aliyeisifia Agrisol, baadhi ya madiwani hatukuruhusiwa kuingia” anasema.
Naye afisa kilimo wa kata hiyo Righton Myombe alisema kuwa hawakuwahi kutangaziwa kuhusu uwekezaji wa eneo hilo,
“Siyo kweli kwamba serikali ilitangaza kwa wakulima kuhusu uwekezaji huo. Sisi tumeshukia tu Agrisol wamekuja na tunatakiwa tushirikiane nao, lakini hatujui faida yake” anasema.
Kwa upande wake mwanaharakati wa mazingira wilayani humo, Masanja Katambi anasema kuwa eneo hilo lilipaswa kugawiwa wafugaji ambao mara nyingi hutaabika kutafuta maeneo ya malisho.
“Mwaka 2009, tulikuwa na kikao na Waziri Mkuu Pinda kuhusu matatizo ya malisho kwa wafugaji, akatuahidi kutupatia eneo rasmi la kufugia. Tulitegemea kwamba wakimbizi wakiondoka tutapata eneo hilo. Sasa tumeshtushwa kuwa kuna Wamarekani wanakuja” anasema Katambi na kuongeza,
“Kwakweli ni janga la kihistoria, itakuwa kama mgodi wa Mwadui (William Diamondson) ambao mkataba wake haukomi hadi leo, wananchi hawaambulii kitu”.
Kwa upande wa kambi ya Mishamo, wanakijiji wanaozunguka kambi hizo nao hwaelewi watafaidikaje na mradi huo.
Afisa Mtendaji wa kata ya Mishamo Augustine Wangagwa anasema kuwa wananchi hawakushirikishwa kwa lolote katika uwekezaji huo, wamekuwa wakisikia sikia tu.
“Tumekuwa tukisikia tu huo uwekezaji, tulitarajia kushirikishwa kuanzia ngazi ya kitongoji. Lakini tunasikia mambo yaliishia kwenye halmashauri tu. Diwani wangu naye alisikia kwenye vikao lakini hakushirikishwa zaidi” anasema.
Hata hivyo Wangagwa anasema kuwa eneo hilo likiachwa baada ya kuondoka wakimbizi, halitatumika ipasavyo kwani wananchi katyika vijiji vinavyozunguka kambi hiyo ni 13,490 ukilinganisha na wakimbizi 58,000 waliopo katika kambi hiyo.
“Hatuna pingamizi, wao waje tu. Kwasababu hata wasipokuja eneo lote hili tutalifanyia nini? Sana sana tunachotaka kujua, tutafaidika nini?” anasema Wangagwa.
Naye Mbunge wa Mpanda Kati Said Arfi anasema kuwa atawasilsha hoja Bungeni kuupinga mkataba huo kwa madai kuwa ni batili.
“Nitawasilisha hoja binafsi katika bunge linalokuja, ili kuitaka serikali isitishe umilikishaji huo. Kama serikali itang’ang’ani, basi, iwatafutie AgriSol, ulinzi wa kutosha, kwani wananchi hawatakubali.
Anasema kuwa wanachokuja kufanya AgriSol ni kilimo cha nishati siyo mazao ya chakula.
“Kinacholengwa hapa ni kilimo cha nishati ya mimea (bio fuel). Hatari kubwa ninayoiona hapa ni kwamba watazalisha mazao hasa mahindi kwaajili ya kupata nishati na kulisha mifugo yao”.
Arfi anasema kuwa hajawahi kushirikishwa kwenye mikutano ya kuwajadili AgriSol, lakini atachukua hatua kwa manufaa ya taifa bila kujali mipaka ya jimbo.

Utata wa kuondoka wakimbizi
Pamoja na jitihada za serikali kuhakikisha kuwa eneo hilo linabaki wazi kwaajili ya kupewa mwekezaji, bado kuna utata wa kuondoka kwa wakimbizi hao.
Kwa mujibu wa Mkuu wa kambi hizo, Athuman Igwe, serikali ilikuwa imewapangia wakimbizi hao kuhamia katika mikoa 16, lakini wengi wamechagua kubaki mkoa wa Rukwa isitoshe wanapinga kulipwa kiasi cha 300,000 wakidai kuwa hakitoshi.
Katibu tawala wa wilaya ya Mpanda anasema kuwa Wakimbizi hao wanataka walipwe sh 2.8 milioni kwa kichwa.

Thursday, June 30, 2011

KWANINI WABUNGE WANALALA SANA BUNGENI?

Tatizo lilianza pale wabunge walipoamua kuhamishia ukumbi wao kutoka Karimjee na kwenda Dodoma ambako walijengewa ukumbi wa Msekwa. Ukumbi wa Msekwa ulikuwa wa kifahari kuliko wa Karimjee. kama hiyo haitoshi wakajenga mwingine wa kifahari zaidi wanaoutumia sasa.
Ukumbi huu wa sasa umejengwa kifahari, ambapo Mbunge akikaa kwenye sofa lake hata kama hajisikii usingizi atalazimika tu kulala kwa jinsi linavyobembeleza. Kuna taarifa kuwa ubunge huu uliogharimu mabilioni ya shilingi kujengwa, unataka kubomolewa ili uongezwe.

Ukiangalia Bunge la Kenya Ukumbi wao hauna tofauti na ule wa Karimjee, japo wao umepambwa zaidi. Lakini Wabunge wanakaa kwenye mabenchi tu. hata kama mtu unausingizi unaweza kushtuliwa na mwenzako. Lakini hii ya mheshimiwa kukaa kama yuko ofisini....


Waziri Steven Wassira akiuchapa usingizi



Mbunge wa Vunjo Augustine Mrema naye yuko ndotoni kabisa




John Komba ndiyo kabisa!







NAPE ALIPOTEMBELEA MWANANCHI

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM akiangalia magazeti yaliyochapishwa katika mitambo iliyopo ofisi za Mwanancho Communication.
Picha ya chini akiwa katika mazungumzo na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi wa Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti.





Monday, May 30, 2011

HE'S BACK

Ilikuwa ni furaha tupu katika familia baada ya First born wa familia David, kurudi nyumbani baada ya miaka 16 ya kuwa ughaibuni. Kwanza tulimshukuru Mungu kanisani, halafu tukarudi nyumbani kusherehekea
Hapa tulikutana Muheza Tanga anakoishi mama.


Feel at home


At church




















It facinates