Wednesday, October 28, 2009

MZEE MTEI AZINDUA KITABU CHA MAISHA YAKE

Gavana wa kwanza wa Tanzania na mwanzilishi wa Chadema, Edwin Mtei, hivi karibuni amezindua kitabu cha wasifu wa maisha yake. Kitabu hicho kina stori ya kusisimua sana kuhusu maisha yake sambamba na utawala wa Nyerere. Utasoma jinsi alivyokorofishana na Nyerere hadi akajiuzulu.
Aliyekizindua ni Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi na kuhudhuriwa na watu mashuhuri na waandishi wa habari.












Tuesday, October 20, 2009

NABII CHAPOMBE


Huyu ndiye Nabii Tito (Cha Pombe) ambayeamekuwa akizunguka mitaa mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam kuwashawishi watu wanywe pombe maana siyo dhambi kufanya hivyo.
Akiwa kwenye anga zake, kabla hajaanza kupiga mahubiri kwanza ana “beha” msuba (anavuta sigara), kisha anaipiga nyundo, ndipo anaanza mahubiri.
Picha hii inamwonyesha akiwa mtaa wa Samora katikati ya jiji la Dar es salaam, akivuta sigara kabla hajaanza mahubiri yake.
Maandiko anayotumia nabii “Chapombe” haya hapa,
1Timotheo 5: 23
1Timotheo 3: 7- 8
Mithali 31: 6- 7
Mhubiri 9: 7- 8
Mwanzo 9: 20- 21
Luka 7: 33 – 35
Luka 22: 14 20
Yohana 2: 1- 11
Tito 2: 3
Wakolosai 2: 10 – 16
Mwanzo 19: 31 – 35

Haya wadau, ukweli ni upi?

Wednesday, October 14, 2009

MIAKA 10 YA INJILI, TANZANIA KWA YESU

Kanisa la Tanzania Assemblies Of God limezindua Mkakati wa kuhubiri injili kwa kasi uitwao, "Miaka 10 ya Injili Tanzania kwa Yesu". Katika picha hizi anaonekana mhubiri aliyetambulika kwa jina la Mrs Lema akihubiri mkutano wa Injili Mburahati jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulipambwa na kwaya mbali mbali.












Sunday, October 11, 2009

SIMON ALIPOJICHUKULIA JIKO LAKE

"Mnaiona hii?" Ndivyo anavyoonekana kusema Mchungaji Mkama wa Kanisa la TAG Ilala aliyekuwa akisajili ndoa kati ya Simon Mmbaga na Joyce Tembo iliyofungwa katika kanisa la TAG Kigogo. Sherehe za harusi hiyo zilifanykia katika ukumbi wa baraza la maaskofu wa Katoliki Kurasini jijini Dar es Salaam.





Nakuvalisha Pete hii.......

Mguu pande.....





Tuesday, October 6, 2009