Tuesday, June 29, 2010
SUGU KUGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CHADEMA
Yule mwasisi wa Muziki wa Bongo flavour, Joseph Mbilinyi aka Mr II au ukipenda mwite Two Proud au hata Sugu, sasa ametangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chadema.
Uamuzi wa mshikaji umekuja siku chache tu tangu alipotiwa mbaroni na jeshi la polisi akidaiwa kutoa wimbo wenye maudhui ya kumtishia kifo Mkurugenzi wa Clouds entertainment, Ruge Mutahaba.
Hata hivyo yeye amekanusha madai hayo akisema kuwa maneno yaliyomo katika wimbo wake huo hasa lile la 'Kill' hayamaanishi kuua bali kuondoa.
Mwenyewe anakichukulia kitendo hicho kama fitna anazofanyiwa na wabaya wake katika kufanikisha malengo yake mbele ya Watanzania.
"Mimi niko katika mapambano, hata kama kesi hizi zitanipeleka jela, basi ndiyo itakuwa mwisho wangu, lakini sijakata tamaa" alisema Sugu katika mahojiano naye tuliyoyafanyia Sinza Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment