Wednesday, October 28, 2009
Gavana wa kwanza wa Tanzania na mwanzilishi wa Chadema, Edwin Mtei, hivi karibuni amezindua kitabu cha wasifu wa maisha yake. Kitabu hicho kina stori ya kusisimua sana kuhusu maisha yake sambamba na utawala wa Nyerere. Utasoma jinsi alivyokorofishana na Nyerere hadi akajiuzulu.
Aliyekizindua ni Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi na kuhudhuriwa na watu mashuhuri na waandishi wa habari.
Aliyekizindua ni Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi na kuhudhuriwa na watu mashuhuri na waandishi wa habari.
Tuesday, October 20, 2009
NABII CHAPOMBE
Huyu ndiye Nabii Tito (Cha Pombe) ambayeamekuwa akizunguka mitaa mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam kuwashawishi watu wanywe pombe maana siyo dhambi kufanya hivyo.
Akiwa kwenye anga zake, kabla hajaanza kupiga mahubiri kwanza ana “beha” msuba (anavuta sigara), kisha anaipiga nyundo, ndipo anaanza mahubiri.
Picha hii inamwonyesha akiwa mtaa wa Samora katikati ya jiji la Dar es salaam, akivuta sigara kabla hajaanza mahubiri yake.
Maandiko anayotumia nabii “Chapombe” haya hapa,
1Timotheo 5: 23
1Timotheo 3: 7- 8
Mithali 31: 6- 7
Mhubiri 9: 7- 8
Mwanzo 9: 20- 21
Luka 7: 33 – 35
Luka 22: 14 20
Yohana 2: 1- 11
Tito 2: 3
Wakolosai 2: 10 – 16
Mwanzo 19: 31 – 35
Haya wadau, ukweli ni upi?
Wednesday, October 14, 2009
MIAKA 10 YA INJILI, TANZANIA KWA YESU
Kanisa la Tanzania Assemblies Of God limezindua Mkakati wa kuhubiri injili kwa kasi uitwao, "Miaka 10 ya Injili Tanzania kwa Yesu". Katika picha hizi anaonekana mhubiri aliyetambulika kwa jina la Mrs Lema akihubiri mkutano wa Injili Mburahati jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulipambwa na kwaya mbali mbali.
Sunday, October 11, 2009
SIMON ALIPOJICHUKULIA JIKO LAKE
Tuesday, October 6, 2009
Subscribe to:
Posts (Atom)