Mtindo mpya aliouanzisha Rais Kikwete wa kuzungumza na wanananchi kupitia vyombo vya habari ambapo sasa wananchi wana fursa ya kupiga simu, kutuma sms na hata e mail, umeonyesha jinsi ambavyo Rais Kikwete yuko karibu na wananchi kinoma.
Rais Kikwete alisema kwamba amegundua kwamba hata hotuba anazozitoa anapokuwa ziarani huwa haziendani kabisa na matakwa ya wananchi, kwahiyo ni bora tu awape nafasi waulize wanachotaka. Tena Kikwete anataka hata wananchi wawe wanakwenda ikulu wanapokuwa na shida,
"Wakati mwingine ninapokuwa Ikulu huwa nawauliza wasaidizi wangu, hivi hakuna wananchi wenye matatizo wanaokuja hapa Ikulu?" aliuliza Rais Kikwete.
Kufuatia hali hiyo Rais Kikwete amepanga kuwa anakutana na wananchi wenye matatizo nje ya Ikulu kama alivyokuw akifanya Mzee ruksa enzi zile.
No comments:
Post a Comment