Friday, September 4, 2009

Chadema Hooray!

Mwenyekiti wa Chadema freeman Mbowe akipongezwa na wanachama wa chama hicho baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kiti hicho.

















MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Freeman Mbowe amefanikiwa kutetea nafasi hiyo kwa mara ya pili baada ya kupata ushindi wakura za ndiyo kwa ailimia 92.9 kutoka kwa wajumbe wa mkutano mkuu uliofanyika jana katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi huo, ambaye pia ni mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Bob Makani alisema kwamba, kura za hapana kwa nafasi hiyo zilikuwa 22 sawa na asilimia 4.8 wakati kura za ndiyo zilikuwa 425 sawa na asilimia 92.9 na kuongeza kuwa kura zilizoharibika ni 10 sawa na asilimia 2.1.


Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, ukumbi ulilipuka kwa shangwe na furaha huku baadhi ya wajumbe wakimvamia Mbowe na kumbeba juu juu mpaka katika meza kuu.

No comments:

Post a Comment