Tuesday, July 20, 2010

CHEKI JINSI AL SHABAB WALIVYO
















BAADA ya kundi la waasi nchini Somalia, Al-Shabab lenye uhusiano na mtandao wa Al Qaida kudai kuhusika na mashambulizi nchini Uganda, sasa limeahidi kuendeleza mashambulizi hayo.
Kiongozi wa kundi hilo, Muhammad Abdi Godane amedai kuhusika na mashambulizi ya mabomu yaliyotokea nchini Uganda hivi karibuni na kusema anapanga mashambulizi zaidi.
Kiongozi wa kundi la waasi wa al Shabaab nchini Somalia ametishia kuendeleza mashambulizi ya kundi hilo nchini Uganda katika siku zijazo. ametoa taarifa hiyo kupitia vituo vya redio mjini Mogadishu na kusisitiza kuwa, kile kilichojiri hivi karibuni mjini Kampala ni mwanzo tu.
“Tutaendelea kukabiliana na maadui wa nje popote walipo. Hakuna atakayetuzuia kutekeleza kazi zetu za kiislamu” anasema Sheik Ali Mohamud Rage, msemaji wa kunpdi hilo mjini Mogadishu.
Mabomu ya Jumapili yameua zaidi ya watu 70 waliokuwa wakiangalia fainali za kombe la dunia kwenye televisheni mjini Kampala.
Kati ya waliouawa ni mfanyakazi wa kutoa misaada wa Marekani pia ameuawa. Wanachama wengine sita wa kanisa kutoka Pennsylvania Marekani walijeruhiwa vibaya katika mlipuko huo uliolengwa nje ya uwanja wa mkahawa wa Kiethiopia mjini Kampala.
Damu na viungo vya binadamu vilikuwa vimetapakaa sakafuni na kwenye viti vilivyopinduliwa na mlipuko huo wakati watu walipiokuwa wakiangalia mechi kati ya Hispania na Uholanzi.
Kamanda wa jeshi la Al-Shabab Yusuf Sheik Issa amefurahia tukio hilo la kwanza kufanywa na kundi hilo nje ya mipaka ya Somalia.
"Uganda ni moja ya maadui zetu, kila kinachowaliza kinatupa furaha. Tunaomba hasira za Allah's ziwe juu ya wote walio kinyume na sisi” anasema Sheikh Issa.
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameapa kujibu vikali. Amesema wanajeshi wa Uganda nchini Somalia wanashughulikia ulinzi, lakini wataanza kulivunja kundi la Al Shabab.

Thursday, July 1, 2010

WABONGO NA KUSAJILI LINE ZA SIMU

Walipotangaza kuongeza muda, watu wakawa hawaendi. siku zilipokaribia kwisha ndiyo wanajazana. Siku zimeongezwa tena, hukuti mtu kwenye usajili, wanasubiri siku za mwisho.

Hata sasa hivi watu wakiambiwa kuwa Yesu atarudi mara ya pili, hawaamini kabisa. Sasa tofauti yake ni kwamba, kwa Mungu hakutakuwa na muda wa nyongeza wa kutubu.