Monday, August 31, 2009

Mwongozo kwa Waislam

Waislamu na mwongozo wao





“Wakatoloki wameanzisha sisi tunamaliza”



Na, Elias Msuya


BAADA ya wakristo wa madhehebu ya Kikatoliki kutoa waraka unaowakata waumini wake wajiandae kwaajili ya uchaguzi wa mwakani, Waislam nao wamekuja na mwongozo wao wenye malengo kama hayo.
Katika mkutano wa uzinduzi wa waraka huo uliofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam, Waislam hao waliokuwa chini ya viongozi wa Shura ya Maimam Tanzania, wameeleza nia yao ya kutoa waraka huo.
Kiongozi wa shura ya Maimamu, Sheikh Issa Ponda, amesema kwamba Waraka huo una vipengele 16 ambavyo vimefafanua vipaumbele vya Waislam.
“Waraka huu una vipengele 16 ambavyo ni Taswira ya Uchaguzi mkuu uliopita, Dhana ya uchaguzi, Uhuru wa kutoa maoni, Tumefukaje hapa tulipo, maadili, Elimu, Afya, kilimo, Fedha na uwezeshaji, maisha bora, sheria, umoja na amani, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, uwakilishi wa umma, hadaa za uchaguzi na dira ya uchaguzi”
Ponda amewataka Waislam kupigania haki zao kwakuwa Waislamu ndiyo walioikomboa nchi hii na ndiyo wako wengi kuliko Wakristo,
“Tumesimama katika uwanja huu (Mnazi Mmoja), kama wazee wetu waliokuwa wakipigania uhuru walipokuwa waikikutana hapa kwaajili ya kupanga mikakati ya kuikomboa nchi. Na sisi tuko tayari kwaajili ya kupigania maslahi ya Uislamu” anasema Ponda.
Mwongozo wenyewe
Kipengele cha kwanza cha mwongozo huo kinaeleza Taswira ya Uchaguzi mkuu uliopita. Kwamujibu wa kipendele hicho, uchaguzi huo ulitawaliwa na ubabe aliokuwa nao Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.
Aidha, vyombo vya usalama navyo vimeelezewa kuingilia shughuli za uchaguzi na kuwanyanyasa wananchi,
“Moja ya matukio mabaya yaliyowasibu wananchi wakati wa kampeni ni lile la Desembe 12,2005 ambapo polisi waliwapiga risasi wananachi wawili Magomeni jijini Dar es Salaam wakiwa wanatoka katika mkutano wa kufunga kampeni za Chama cha Wananchi CUF".
Taasisi za umma nazo zimenyooshewa kidole kwa kuipigia debe CCM wazi wazi. Taasisi hizo ni pamoja na vyombo vya habari kama vile radio na televisheni kushabikia mgombea wa CCM kuliko wagombea wa vyama vingine.
Katika zoezi la kupiga kura, kipengele hicho kimebainisha kwamba wananchi wengi walinyimwa nafasi ya kupiga kura kwa kukosa majina yao kwenye Daftari la Kudumu la wapiga kura.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imelalamikiwa kwa kuwanyima haki Waislamu kusimamia uchaguzi huo.
“Kamati kuu ya siasa ya Shura ya Maimamu Tanzania ilimwandikia Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuomba kuruhusiwa kuweka waangalizi katika majimbo yote ya uchaguzi nchini….(Awali majibu yalikubaliwa) “hata hivyo katika hali isiyotarajiwa…Mkurugenzi wa uchaguzi Rajab Kiravu aliiandikia barua Shura kubatiolisha kukubaliwa kwao….”
Kipengele cha pili kinahusu Dhana ya uchaguzi. Dhana hiyo imeelezewa kwamba japo waislamu ni wengi wamekuwa wakipiga kura kwa maslahi ya Taifa bila kujali makundi makubwa ya kidini ya Waislamu na Wakristo. Lakini akristo wao wamekuwa wakipiga kura kwa maslahi yao.“Kutokana na mazingatio haya karibu viongozi wote wanaochaguliwa hata wale ambao ni Waislamu wamejikuta wakiendesha shughuli za kila siku za nchi kwa kuzingatia maelekezo na maslahi ya kanisa na Wakristo” inasema sehemu ya Waraka huo.
Katika kipengele cha uhuru wa kutoa maoni, mwongozo umeeleza kitendo cha Wakristo wa madhehebu ya Wakatoliki kutoa waraka wao. Kitendo hicho kimeelezwa kuwa kama mbinu ya Wakristo kuwateka kimawazo viongozi wa serikali.
“Katika jitihada za kuhakikisha tunu za kikiristo zinaonekana katika sera na bajeti za serikali, Februari 21, 2009, Maaskofu walikutana na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete katika hafla ya kidini. Wengine waliokuwepo ni pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta, Jaji Mkuu, Agustino Ramadhan na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi. Katika mazungumzo yao, kadinali Polycarp Pengo aliwakumbusha waumini wao kuelekeza kwa wagombea urais Ubunge na udiwani na chama chenye maslahi kwao.”
Mwongozo katika kipengele hicho umewataka Waislamu kufanya zoezi la uchaguzi kuwa kama ibada yao kama wafanyavyo Wakristo.
Kwa mujibu wa waraka huo, nchi yetu imefika hapo ilipo kutokana na makubaliano rasmi kati ya serikali na kanisa.
“kwa kutumia mapinduzi ya kimya kimya, kanisa limefanikiwa kuitumia mno serikali kwa maslahi yake, kiasi cha kufunga mikataba mikubwa ya kudhulumu raia wa jamii ya wengine wasiokuwa wakristo. Mfano hai ni ule mkataba wa mwaka 1992 ujulikanao kama “Memorandum of Understand between Christian council fo Tanzania and Tanzania Episcopal Conference and the United Republic of Tanzania (MoU)”
Kwa mujibu wa mkataba huu, baadhi ya majukumu ya kanisa yamekasimishwa kufanywa na kanisa huku serikali ikiwa ndiyo mfadhili wa kutoa mabilioni ya kodi za wananchi kuwezesha miradi mbali mbali ya makanisa.
Kipengele hicho kinefafanua kwamba dini ya Kiislamu imekuwa ikihujumia na serikali tangu tulipopata uhuru.
“Utekelezaji wa mkakati wa kuapambana na adui ‘uislamu’ ulinza rasmi mwaka 1963. Mwaka huo… Mwalimu Nyerere alitumia madaraka yake kama rais kuifuta mahakama ya kadhi. Mwaka 1964 Nyerere alitumia kisingizio cha maasi ya kijeshi kuwahujumu viongozi wa kiislamu akiwamo Mufti Sheikh Hassan bin Amir kwa kuwahusisha nao.
Mwaka 1968 Nyerere aliendesha vitisho vingi dhidi ya Masheikh, akaivunja jumuiya ya Waislam ya East African Muslim Welfare society Society (EAMWS) tawi la Tanzania na kuunda Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA)”.
Katika suala la maadili, mwongozo huo umejadili kuwepo kwa ubaguzi kati ya wakristo na waislamu nchini hasa katika masuala ya elimu na ajira.
“Kwa ujumla kiasi cha asilimia 80 ya fursa zote za elimu na ajira zinachukuliwa na Wakristo, mara nyingi kwa njia ya upendeleo.”
Aidha kipengele hicho pia kimejadili kuwepo kwa ubabaishaji katika serikali na hivyo kutokea kwa kashfa za wizi,rushwa, ulaghai na ubadhirifu kwa viongozi wa serikali.
Dhana ya uongozi imepotoshwa na sasa uongozi umekuwa ni gari la kuendeshea maslahi binafsi na kuliko kuhangaika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo ya kweli.
Suala la maadili katika shule pia limepuuzwa ambapo wanafunzi wamekuwa wakiruhusiwa kuvaa mavazi ya ajabu. Maeneo ya vyuo yamegeuzwa kuwa kama casino kwa ulevi na ngono.
Katika ajira, watendaji katika ofisi wamegeuza ofisi zao kuwa kama minada ya kuuza huduma za jamii.
Katika sula la elimu, mwongozo huo umeonyesha jinsi ambao Wakristo walivyoshikilia nyanja hiyo.
“Kwa msingi huu, makanisa yanamiliki zaidi ya vyuo vikuu vinane na vyuo vikuu zaidi ya 11. Pia wamekuwa wakihodhi na kuatamia wizara ya Elimu na Baraza la Mitihani kwa miaka yote.”
Kwa upande wa Afya mwongozo pia umeonyesha jinsi Waislamu walivyonyimwa haki ya kumiliki huduma za afya. Wakristo wamedaiwa kumiliki hospitali teule na zile za rufaa wakati Waislam hawana fursa kama hizo.
Waislamu pia wametakiwa kuutumia uchaguzi ujao kwa kuchagua viongozi watakaohakikisha kuwa wanahamasisha kwa unguvu uanzishwaji wa mabenki yanayoendeshwa kwa kanuni za Kiislamu ili kuongeza uzalishaji na kupanua ajira kwa vijana nchini.
Katika kipengele cha maisha bora, mwongozo huo umesema kwamba maisha bora yanakosekana kutokana na nchi hii kutawaliwa na viongozi wa kikatoliki kwa asilimia 80. Hivyo waislamu wametakiwa kuchagua viongozi wenye dhamira ya kuboresha maisha na ustawi wa wananchi.
Katika suala la sheria, mwongozo huo umepinga kupitishwa kwa sheria ya ugaidi ambayo inaonekana kuwanyanyasa Waislamu. Aidha mwongozo huo pia umeonyesha jinsi ambavyo sheria za Tanzania ziazvyowabagua Waislamu.
Mwongozo pia umesikitishwa na kitendo cha serikali kukataa maombi ya Waislamu ya kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi pamoja na Tanzania kujiunga na Jumuiya ya nchi za kiislam (OIC) kama wakatoliki walivyojiunga na Vatcan.
Mwongozo huo pia umejadili masuala ya Umoja na amani, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, uwakilishi wa umma, hadaa za uchaguzi na dira yetu katika uchaguzi.




Si mchezo!

No comments:

Post a Comment